KUHUSU AMP

JE, UTAFITI WA AMP NI NINI?

AMP humaanisha Uzuiaji Unaowezeshwa na Fungomwili (Antibody Mediated Prevention). Hii ni dhana ya kuwapa watu kingamwili ili kubaini kama zitawalinda watu dhidi ya kuambukizwa HIV.

Utafiti wa AMP ni dhana mpya ya kuzuia HIV ambayo inahusiana na kile kilichofanywa katika uchunguzi wa chanjo ya HIV. Katika utafiti wa kawaida wa chanjo ya HIV, watu hupata chanjo na watafiti husubiri kuona ikiwa miili yao itatengeneza kingamwili dhidi ya HIV. Katika utafiti huu, tutaruka hatua hiyo, na kuwapa watu kingamwili moja kwa moja. Tutafanya hivi kwa kudunga katika mishipa ya damu, inayojulikana kwa kawaida kama “IV” au “kupata dripu”. Huu ndio utafiti wa kwanza unaopima kama kingamwili zinaweza kuzuia maambukizo ya HIV katika watu.

JE, FUNGOMWILI HII NI NINI?

Fungomwili ni protini halisi mwilini ambazo hukabiliana na magonjwa. Zinaweza kujibandika nje ya bakteria na virusi ili kuzizuia dhidi ya kusababisha maambukizo. (Hii inaitwa "kukabiliana.") Unaweza kuchukulia kuhusu fungomwili kama askari wa mwili, wanaofanya kazi kulinda watu dhidi ya maambukizo. Fungomwili hii, inayoitwa VRC01, ni fungomwili inayokabiliana na aina nyingi za virusi vya HIV. Majaribio ya maabarani yameonyesha kwamba fungomwili zinazokabiliana na aina nyingi za virusi kama vile VRC01 zinaweza kuzuia maambukizo yanayotokana na aina nyingi tofauti za HIV kutoka duniani kote. Zinafanya hivi kwa kujibandika kwenye maeneo ya virusi ambayo virusi hutumia kujibandika kwenye seli zenye afya, kwa hivyo kuzuia maambukizo. Utafiti wa AMP utatusaidia kujua kama fungomwili ya VRC01 itazuia maambukizo ya HIV katika watu. 

VRC01 / HIV Virus Attachment from HIV Vaccine Trials Network on Vimeo.

Nieleze zaidi kuhusu IV au dripu.

IV au dripu huanza kwa mfuko wa myeyusho wa kawaida wa chumvi na maji, sawa na maji ya chumvi ambayo hupewa watu waliopungukiwa na maji mwilini. Fungomwili ya VRC01 huongezwa kwenye myeyusho wa chumvi na maji na mfamasia. Kiasi cha fungomwili ambacho huongezwa hutegemea uzani wa mshiriki katika utafiti, kwa hivyo wale wenye uzani zaidi hupata fungomwili zaidi. Vipimo viwili vya fungomwili vitajaribiwa ili kuona kama vinaweza kufanya kazi ya kuzuia maambukizo ya HIV: kipimo cha 10/mg/kg na kipimo cha 30 mg/kg. Baadhi ya watu watapata kipozaungo, ambacho kina myeyusho wa kawaida wa chumvi na maji bila kuongezwa fungomwili. IV au dripu hupewa mshiriki katika utafiti kwa dakika 30-60. Ili kupewa IV, sindano safi hutumiwa kuweka tyubu ndogo ya plastiki kwenye mshipa wa mkono wa mshiriki. Mfuko wenye kioevu huangikwa kwenye ncha na kuunganishwa kwenye pampu, ambayo hudhibiti jinsi yaliyomo kwenye mfuko yatatiririka kwenye tyubu hadi ndani ya mkono wa mshiriki.

Je, ni nani anayetekeleza utafiti huu?

Utafiti unatekelezwa na vikundi viwili, Mtandao wa Majaribio ya Chanjo ya HIV na Mtandao wa Majaribio ya Kuzuia HIV. Mashirika haya yote na kliniki zote husika za utafiti zinafanya kazi kwa pamoja na washikadau wa jamii ili kuhakikisha kwamba utafiti huu unakubalika katika jamii ya eneo husika na unaheshimu utamaduni wa jamii husika.