KUJITOLEA

UNACHOPASWA KUTARAJIA UKIAMUA KUJITOLEA

Tutajibu maswali yoyote ambayo unayo ili kuhakikisha unaelewa kinachofanika unaposhiriki katika utafiti wetu

  •  Utapimwa mwili, vipimo ambavyo vinahusisha kupimwa damu.
  • Wakati wa utafiti huu, utadungwa IV 10, mara moja kila wiki 8. Hii huchukua dakika 30-60. Zinaweza kuwa na fungomwili ya utafiti, au zinaweza kuwa na kipozaungo (isiyofanya kazi)
  • Utaombwa ufuatilie jinsi unavyohisi kwa siku 3 kufuatia kila IV. Utakuwa ukiwasiliana na mhudumu wa kliniki kuhusu unavyohisi wakati huu.
  • Ziara za kufuatilia zitajumuisha ushauri na vipimo vya HIV, na kujibu maswali kutoka kwa wahudumu wa kliniki. Ziara hizi zitakuwa fupi kuliko ziara ambazo unapewa IV.