UKURASA WA MWANZO

Wachunguzaji wa AMP watangaza matokeo ya kwanza kutoka Kwa Tafiti za AMP 


AMP humaanisha Uzuiaji Unaowezeshwa na Fungomwili (Antibody Mediated Prevention). Hii ni dhana ya kuwapa watu fungomwili ili kubaini kama zitawalinda watu dhidi ya kuambukizwa HIV.

Utafiti huu, pia unaorejelewa kama HVTN 703/HPTN 081, unajaribu dhana mpya ya kuzuia HIV. Katika utafiti wa kawaida wa chanjo, tunawapa watu chanjo na kusubiri kuona ikiwa miili yao itatengeneza fungomwili dhidi ya HIV. Katika utafiti huu, tutaruka hatua hiyo, na kuwapa watu fungomwili moja kwa moja. Tutafanya hivi kwa kuidunga fungomwili mishipa ya damu, ambayo baadhi ya watu wanaifahamu vyema kama kupewa IV au dripu. Huu ndio utafiti wa kwanza unaopima kama fungomwili zinaweza kuzuia maambukizo ya HIV katika watu.