Utafiti huu unatarajiwa kuanza kuandikisha washiriki mwaka wa 2016. Utafiti huu utafanyika katika maeneo yafuatayo barani Afrika:
Utafiti mwingine wa AMP unaofanana sana na utafiti huu unafanywa nchini Marekani na Amerika Kusini. Utafiti huu pia unatarajiwa kuanza kuandikisha washiriki mwaka wa 2016. Utafiti huo mwingine wa AMP unajulikana kama HVTN 704/HPTN 085.
Taasisi ya Kitaifa ya Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza (NIAID), ambayo ni sehemu ya Taasisi za Kitaifa za Afya Marekani, inalipia utafiti huu. NIAID, Mtandao wa Majaribio ya Chanjo ya HIV (HVTN), na Mtandao wa Majaribio ya Kuzuia HIV (HPTN) umeandaa utafiti huu. Kituo cha Utafiti wa Chanjo cha Dale and Betty Bumpers (VRC), ambacho ni sehemu ya NIAID, kinatoa fungomwili ya VRC01 kwa utafiti huu.
HVTN na HPTN zote ni ushirikiano wa kimataifa wa wanasayansi, waelimishaji na wanajamii wanaotafuta njia mwafaka za kuzuia HIV. HVTN huzingatia kupata chanjo salama na mwafaka za HIV, nayo HPTN huzingatia mbinu nyingine za kuzuia HIV, kama vile uzuiaji wa kabla ya kuhatarishwa na matibabu kama njia ya kuzuia. HVTN imefadhiliwa na NIAID. HPTN imefadhiliwa kwa ushirikiano wa NIAID, Taasisi ya Kitaifa kuhusu Utumiaji Dawa za Kulevya (NIDA), na Taasisi ya Kitaifa ya Afya ya Akili (NIMH).
Tafiti zote za HVTN na HPTN hushirikiana kutimiza dhamira ya pamoja ya kugundua mbinu mwafaka za kuzuia maambukizo ya HIV. Lengo kuu la utafiti huu ni:
VRC01 itapeanwa kwa kudungwa ndani ya mishipa ya damu. Njia hii ni maarufu kama kudungwa sindano ya mishipa ama kudungwa dawa kwa matone. Mshiriki wa utafiti hudungwa sindano ya mishipa kwa dakika 15-60. Ili kudunga sindano ya mishipa, sindano iliyosafishwa kabisa hutumiwa kutia mrija mdogo wa plastiki ndani ya mshipa mkononi mwa mshiriki. Mfuko wa kiowevu huanikwa kwenye kikingi na kuunganishwa kwenye pampu ambayo hudhibiti kasi ya mtiririko wa kiowevu kilicho kutoka mfukoni kupitia mrija hadi ndani ya mkono wa mshiriki.
Kutakuwa na vikundi 3 tofauti katika utafiti huu. Theluthi moja ya washiriki wa utafiti watapokea kipimo kikubwa zaidi cha fungomwili katika sindano ya mishipa. Theluthi moja ya washiriki wa utafiti watapokea kipimo kidogo zaidi cha fungomwili katika sindano ya mishipa. Thuluthi moja ya washiriki watadungwa maji safi ya chumvi bila fungomwili yoyote. Hii hujulukana kama fungomwili.
Utafiti huu utawasajili na kuwafuatilia takriban wanawake 1900 katika vituo vya utafiti barani Afrika.
Wanawake wa mataifa ya kusini mwa jangwa Sahara ni miongoni mwa watu walio katika hatari ya juu zaidi ya kuambukizwa. Wanawake hawa wana mahitaji makubwa zaidi ya zana mpya za kuzuia maambukizo ya HIV, na ni muhimu kuwajumuisha katika tafiti zinazotafuta mbinu mpya za uzuiaji.
Ili kujiunga na utafiti huu, ni sharti mwanamke awe mwenye afya nzuri, wa umri wa kati ya miaka 18 na 40, na asiye na virusi vya HIV. Inampasa mwanamke anayeshiriki asiwe mjamzito au anayenyonyesha. Pia kuna vigezo vingine vinavyofaa kutimizwa. Tutawauliza watu kuhusu historia yao ya kimatibabu, tuwafanyie uchunguzi wa mwili na pia tupime sampuli za damu na mkojo wao. Pia tutawauliza watu kuhusu maisha yao ya ngono na matumizi ya dawa katika siku za hivi majuzi.
Hatujui hatari zote za VRC01 kwa sababu imepeanwa kwa takriban watu 140 katika tafiti za awali. Ingawa hakuna mtu yeyote katika tafiti hizo aliyepata tatizo lolote kubwa la kiafya lililohusiana na fungomwili hii, daima kuna uwezekano wa matatizo yasiyotarajiwa.
Ndio maana lengo moja la utafiti huu ni kutambua kama chanjo ya utafiti ni salama kupeanwa kwa watu zaidi. Afya ya kila mshiriki itafuatiliwa vizuri katika kipindi chote cha utafiti.
Hatujui. Tafiti za AMP ni za kwanza zilizoundwa kubaini kama fungomwili ya VRC01 huzuia maambukizo ya HIV. Washiriki wasitarajie kukingwa dhidi ya HIV kwa kushiriki katika utafiti huu wa AMP. Hakika, theluthi moja ya washiriki watapokea kipozaungo.
Washiriki wote wa utafiti huu watashauriwa kuhusu njia za kupunguza hatari ya kuambukizwa HIV.
Wakijadiliana kuhusu mbinu za kupunguza hatari ya kuambukizwa HIV, washiriki na washauri watazungumza kuhusu mambo kama vile kutumia kondomu, matibabu ya kabla ya kuambukizwa, kuepuka pombe na dawa za kulevya wakati wa kushiriki ngono, kupunguza idadi ya wapenzi na kuzungumza na wapenzi watarajiwa kuhusu hali ya HIV. Washauri pia wanaweza kuwapa washiriki maelezo kuhusu ufikiaji matibabu ya kabla ya kuambukizwa katika eneo wanaloishi.
Washiriki wa utafiti huu watachaguliwa bila utaratibu maalum. Hii inamaanisha kwamba utaratibu wa kupokea kipimo kikubwa zaidi cha fungomwili, kipimo kidogo zaidi cha fungomwili au kipozaungo haufanywi kwa utaratibu maalum, ni kama kubahatisha tu. Utaratibu wa kubahatisha hufanywa ili watu walio katika vikundi vitatu wapate nafasi sawa. Washiriki walio katika vikundi vyote vitatu watapata aina sawa ya ushauri wa kibinafsi ili kupunguza hatari ya HIV, kwa hivyo hatari ya kuambukizwa inatarajiwa kuwa sawa katika vikundi vyote. Tunajua kwamba bado wataambukizwa HIV licha ya juhudi za kupunguza hatari ya kuambukizwa. Tofauti kuu baina ya vikundi vya utafiti ni ikiwa watu watapewa fungomwili ya VRC01 au kipozaungo. Kwa sababu kila kitu ni sawa baina ya vikundi ni sawa, tofauti yoyote ya maambukizo ya HIV baina ya vikundi huenda itasababishwa na fungomwili.
Utafiti unatarajiwa kuchukua takriban miaka 5 kwa jumla. Kila mshiriki atakuwa katika utafiti huu kwa kipindi cha karibu miaka 2.
Kwa sasa hakuna mipango ya kuendelea kuwapa washiriki fungomwili baada ya utafiti au kutafuta leseni ili kuitoa kwa umma. Badala yake, tutatumia ugunduzi tutatakaofanya katika utafiti huu:
Hapana, hatutarajii watu watambuliwe na HIV baada ya kufanyiwa vipimo vya kawaida vya HIV. Sampuli za damu ya binadamu iliyo na VRC01 imepimwa kwa kutumia vifaa mbalimbali vya kupima HIV kubaini kama kupewa VRC01 kunaweza kusababisha kutambuliwa na HIV. Katika vipimo hivi vya maabarani, matokeo haya hayakupatikana. Vipimo zaidi vinafanywa kuthibitisha matokeo haya.
Kulinda afya na kuheshimu haki za washiriki ni malengo makuu ya kila mmoja katika HVTN na HPTN. Bila watu wa kujitoa, haiwezekani kupata mbinu mpya za kuzuia maambukizo ya HIV.
Hatua ya kwanza katika kulinda haki za washiriki wa utafiti huu ni kuwapa maelezo kuhusu utafiti kabla ya kujiunga. Utaratibu huu hujulikana kama kutoa idhini. Wahudumu wa kituo watawaeleza watu kuhusu fungomwili hii na taratibu za utafiti huu, hatari na manufaa tarajiwa kwa washiriki, na haki zao. Hizi zinahusisha haki ya kupokea maelezo yoyote mapya kuhusu utafiti, yanayoweza kubaini kama wangependa kuendelea kushiriki, na haki ya kujiondoa kwenye utafiti wakati wowote.
Wakati wa utafiti huu, wahudumu wa kituo watawafuatilia washiriki ili kuhakikisha kwamba fungomwili hii haisababishi matatizo ya afya. Wahudumu wa kituo watawauliza washiriki kuhusu matatizo yoyote ya kijamii yanayoweza kuwakabili kwa kushiriki katika utafiti huu. Ikiwa mshiriki ana tatizo la kiafya au kijamii linalohusiana na utafiti huu, wahudumu wa kituo watamsaidia.
Pia kuna makundi mbalimbali yanayohusika katika kulinda haki na afya ya wahusika:
Kuhusu Utafiti wa AMP: www.ampstudy.org.za
Kuhusu Mtandao wa Majarabio ya Chanjo ya HIV: www.hvtn.org
Kuhusu Mtandao wa Majarabio ya Kuzuia HIV: www.hptn.org
Ikiwa una maswali zaidi ambayo hukujibiwa katika hati hii, tafadhali tuulize. Unaweza kuwasiliana na: [email protected]