Tafiti za AMP zilionyesha kwamba fungomwili ya VRC01 ya monoklonali inayokabiliana na aina nyingi za virusi inaweza kuzuia maambukizi ya aina fulani ya HIV.

  • Hata hivyo, sindano za VRC01 za AMP hazikutoa kinga muhimu kitakwimu za maambukizi ya HIV kwa ujumla.
  • Hii humaanisha kwamba huenda tukahitajika kutumia zaidi ya fungomwili moja ili kufikia kinga mwafaka ya dawa ya HIV.

Tafiti za AMP zilianza kikamilifu mnamo Oktoba 2018. Jozi ya majaribio ya kitabibu ya Awamu ya 2b iliyoendeshwa na Mtandao wa Majaribio ya Chanjo ya HIV (HVTN) na Mtandao wa Majaribio ya Kuzuia HIV (HPTN) iliwasajili washiriki 4,625 walio katika hatari ya maambukizi ya HIV kutoka jamii za Marekani ya Kaskazini na Kusini, Ulaya, na Afrika kusini mwa Sahara.

Tafiti zinaendelea na zitasalia za siri hadi washiriki wote wakamilishe ziara zao za mwisho za utafiti, ambazo zinatarajiwa mapema mwaka wa 2021.

Maelezo zaidi kuhusu Tafiti za AMP na matokeo yake yanaweza kupatikana hapa: